Habari Zetu :

Home » , » DR. SLAA AMFUNDA MANGULA

DR. SLAA AMFUNDA MANGULA

Written By Unknown on Friday, November 30, 2012 | 3:27 AM

DR. SLAA AMPA SOMO MANGULA.....PATA HABARI KAMILI

SIKU chache baada ya Makamu Mwenyekiti mpya wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Philip Mangula, kujibu mapigo ya wapinzani wake akisema wanaombeza wanasahau historia yake, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, amemtaka aweke mikakati hiyo katika vitendo.

Dk. Slaa alidai kuwa kwa sasa Watanzania wamechoka kusikiliza historia, hivyo kama Mangula ana uthubutu aanze kusafisha chama chake kwa kuwaondoa watuhumiwa magwiji wa ufisadi kabla ya kuhangaika na wale waliotoa rushwa kwenye uchaguzi wao. Wakati Dk. Slaa akitoa somo hilo kwa Mangula, naye mwanasiasa mkongwe nchini, Thomas Nyimbo, amemvaa kigogo huyo wa CCM akisema kuwa ni kama anashindana na kivuli chake kwa kujidanganya kuwa ataitokomeza rushwa ndani ya chama hicho.

Kauli hizo zinakuja siku chache baada ya Mangula kakaririwa na vyombo vya habari akitamba kuwa wanaombeza kuwa hawezi kuitokomeza rushwa CCM wanasahau rekodi yake akiwa Katibu Mkuu wa chama hicho. Mangula bila kumung’unya maneno aliwataja wafanyabiashara Yusuf Manji na Thomas Nyimbo kuwa ni miongoni mwa watu aliowafutia ushindi wasigombee ubunge baada ya kubainika kujihusisha na rushwa katika kura za maoni mwaka 2000.

Mwanasiasa huyo pia alikumbushia jinsi chama kilivyofuta matokeo ya baadhi ya washindi katika majibo 32 na kuamuru uchaguzi urudiwe baada ya kubaini uwepo wa mizengwe ya rushwa, hivyo akaahidi kuwa wanaombeza wangoje waone ndani ya miezi sita atakavyochukua hatua. Hata hivyo, katika mahojiano yake na gazeti hili jana, Dk. Slaa aliendelea kumbeza Mangula akisema kama anajisifu kuwa anaweza kuondoa wala rushwa katika CCM, basi aanze na watuhimiwa sugu walioshindikana kung’oka kwenye falsafa ya kujivua gamba.

Alisisitiza kuwa anamshangaa Mangula kwa kujisifu kwa jambo hilo, na kwamba kama kweli anaweza basi atekeleze sera ya kujivua magamba iliyomshinda mtangulizi wake Pius Msekwa na Wilson Mukama. Alisema kuwa watuhumiwa wa ufisadi ndani ya chama hicho ambao wametajwa hadi na wana-CCM wenyewe bado wapo na wanaendelea vema na kazi za kila siku. “Hivyo kama Mangula ana ubavu aanze na hawa aache kujisifia historia, mambo anayoyataja kwanza Watanzania wengi hawayajui, wanataka kuona sasa,” alisema.

Nyimbo ajibu mapigo

Akizungumza na Tanzania Daima kwa simu jana, Nyimbo alisema kitendo cha Mangula kumzungumzia mtu binafsi katika tatizo linalohitaji marekebisho ya mfumo mzima ni suala la kushangaza na kuonyesha kushindwa mapema. “Mangula amepewa nafasi, sasa kama atasema hawezi kutokomeza rushwa japo suala hilo ni la kihistoria unafikiri wanachama wake watamuelewa, si watamshangaa?” alihoji.

Nyimbo aliongeza kuwa historia ya rushwa ilikuwepo hata kwa manabii na kueleza kwamba kinachoweza kufanyika ni kupunguza tatizo kwa kuhakikisha wananchi hawaathiriwi kwa kiasi kikubwa. Kuhusu kuenguliwa kugombea ubunge ndani ya CCM kwa tuhuma za rushwa, kada huyo ambaye aliwahi kuhamia CHADEMA na kujitoa hivi karibuni na kubakia mwanasiasa huru, Mangula alimtaka Mangula kuwa mkweli juu ya hilo.

“Nyimbo ni mwanasiasa mwenye historia yenye kutukuka katika Tanzania huwezi ukanikuta katika kashfa yoyote; sasa huyo ndugu yangu anaposema aliniengua wakati huo alikuwa kiongozi wa wapi?”
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

PROFESSIONAL BLOG DESIGNERS

PROFESSIONAL BLOG DESIGNERS

IDADI YA WATU

BLOG ARCHIVE

DROP YOUR COMMENTS HERE

 
Designed by : Bongo Blogs Designers | Bloggerized by | Tryphone Chasama Jr
Contacts: 0719 625003 / 0765 860437Welcome
Copyright © 2011. SNOUT HOT NEWZ - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template