Katibu
Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii anakaribisha maombi ya kujiunga
na kozi mbalimbali zinazotolewa katika vyuo vinavyoendeshwa na Wizara ya
Afya kwa mwaka wa masomo 2014/2015.
1. Kozi zinazotangazwa ni:
A. Kozi za ngazi ya Stashahada (Ordinary Diploma Programmes):
- Stashahada ya Afya ya Mazingira (Ordinary Diploma in Environmental Health Sciences)
- Stashahada ya Uzoeza viungo (Ordinary Diploma in Physiotherapy )
- Stashahada ya Teknologia ya Viungo Bandia vya Kinywa na Meno (Ordinary Diploma in Dental Laboratory Technology)
- Stashahada ya Teknologia ya Maabara za Afya ya Binadamu (Ordinary Diploma in Health Laboratory Technology)
- Stashahada ya Optometria (Ordinary Diploma in Optometry)
- Stashahada ya Utabibu wa Magonjwa ya Binadamu (Ordinary Diploma in Clinical Medicine)
- Stashahada ya Utabibu wa Magonjwa ya Kinywa na Meno (Ordinary Diploma in Clinical Dentistry)
- Stashahada ya Uuguzi (Ordinary Diploma in Nursing)
B. Kozi za ngazi ya Cheti (Technician Certificate Programme)
- Astashahada ya Teknologia ya Maabara za Afya ya Binadamu (Technician Certificate in Health Laboratory Technology)
- Astashahada ya Utabibu wa Magonjwa ya Binadamu (Technician Certificate in Clinical Medicine)
- Astashahada ya Uuguzi (Technician Certificate in Nursing)
- Astashahada ya Teknologia ya Kutunza Kumbukumbu za Afya ya Binadamu (TechnicianCertificate in Health Record Technology)
- Astashahada ya Afya ya mazingira )Technician certificate in Environmental health Sciences)
2. Muda wa Mafunzo:
i. Miaka mitatu (3) kwa kozi za Stashahada (Ordinary Diploma Programmes)
ii. Miaka miwili (2) kwa kozi za Ngazi ya cheti (Technician Certificate Programmes)
3. Sifa za Muombaji:
Waombaji watarajali (Pre-service):
i. Awe raia wa Tanzania
ii. Awe amemaliza kidato cha nne kati ya mwaka 2009 na 2013, sifa hii inatumika kwawanaotaka kujiunga katika vyuo vya serikakli tu
iii. Cheti
chake cha kidato cha nne, kionyeshe ufaulu wa jumla usiopungua point 28
kwamatokeo ya mwaka 2012 kurudi nyuma na point 35 kwa matokeo ya mwaka
2013.
iv. Ufaulu
wa kidato cha nne uwe wa kiwango kisichopungua alama ya ‘C’, kwa masomo
ya biologia na kemia , na alama ‘D’ kwa somo la fizikia kwa kozi za
Stashahada (Ordinary Diploma) .
v. Ufaulu
wa kidato cha nne uwe wa kiwango kisichopungua alama ya ‘D’, kwa masomo
yabiologia, kemia , na Fizikia kwa kozi za Astashahada (Technician
Certificates)
vi. Kufaulu somo la Kiingereza na Hisabati ni sifa ya nyongeza.
4. Utaratibu wa kutuma maombi:
1. Maombi
yatatumwa na kupokelewa kupitia Mfumo wa pamoja wa kielektronic wa
kupokea nakuchakata maombi [Central Admission System (CAS)] Unaosimamiwa
na Baraza la Elimu ya Ufundi (NACTE). Aidha mfumo huu unapatikana
kupitia kwenye tovuti ya NACTE (www.nacte.go.tz) na tovuti ya wizara ya Afya (www.moh.go.tz) au tovuti maalum ya maombi hayo (www.cas.ac.tz)
2. Waombaji
wote watalipia maombi kupitia mtandao wa M-PESA kwa sh. 30, 000/=.
Kiasi hiki cha fedha hakitarejeshwa (Non refundable). Utaratibu wa namna
ya kulipia na kuomba umeainishwa hapa chini:-
Fuata hatua kama zilivyo hapa chini:
- Kutoka katika simu yako ya mtandao wa Vodacom piga*150*00#
- Chagua 4. Payments (Malipo)
- Chagua 4. Enter business number (Ingiza namba ya Biashara)
- Ingiza namba ya Biashara (Enter the business number) -607070
- Weka nambari ya Kumbukumbu (Enter reference No.) -1234
- Weka Kiasi Cha Malipo (Enter Amount) –30,000
- Ingiza namba ya siri (Enter PIN)
- Ingiza 1 kuthibitisha (Press 1 to Confirm):
Baada
ya Kuthibitisha malipo hayo, utapata ujumbe kutoka Vodacom (e.g.
“Q32LS981 Confirmed. Tshs. 30,000 sent to business NACTE for account
1234 on 14/4/14 at 2:33 PM New M-Pesa balance is....”).
*Tumia namba hiyo ya uthibitisho wa malipo kujaza katika usajili wa mfumo wa CAS [payment details text box(Q32LS981)].
· Bonyeza “submit”, Ujumbe mfupi utatokea kuthibitisha usajili wako katika mfumo wa CAS.
· Bonyeza “Proceed with Admission” kama taarifa zako ni sahihi au “Edit registration details” kama taarifa zako zina kasoro na unahitaji kusahihisha.
5. Namna ya kuomba kujiunga na kozi za Afya kupitia mfumo wa pamoja wa kupokea na kuchakata maombi (CAS).
Hatua za kufuata wakati wa kutuma maombi kwa njia ya elektronic (Online Application Steps)
· Fungua tovuti maalum ya NACTE (http://www.cas.ac.tz)
· Bonyeza “Health Programs ( CertificateauDiploma)”ili kuufungua Mfumo.
· Mfumo wa CAS ukishafunguka kabla hujaendelea utaona michepuko (links) miwili yaani“Home”na“Register”; Kisha
· Bonyeza“Register”na
baada ya kubonyeza na mfumo kukuruhusu endelea kwa kusoma
malekezo,kisha jibu maswali yanayohusu sifa za muombaji (eligibility
questions), baada ya kujibu maswali ya eneo hili Kisha bonyeza “Next”. Kisha endelea kufuata maelekezo utakayokuwa unapewa na mfumo wakati ukiwasilisha maombi yako.
6. Utaratibu
wa kuomba udhamini wa masomo kwa watakaojiunga katika vyuo vya Afya.
Umma unafahamishwa kwamba kwa mwaka huu wa masomo Serikali, kupitia
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa udhamini wa Mfuko wa Fedha wa
Dunia (Global Fund) itadhamini wanafunzi 1401. Taasisi ya Benjamin
William Mkapa (Benjamin Mkapa Foundation) itadhamini wanafunzi 581
miongoni mwa nafasi zilizotengewa udhamini, na Wizara ya Afya na Ustawi
wa Jamii itadhamini wanafunzi 820. Watakaodahiliwa kusomea Mafunzo ya
Ngazi ya Astashahada katika fani zifuatazo:
· Astashahada ya Uuguzi (Technician Certificate in Nursing) - 931;
· Astashahada ya Utabibu (Technician Certificate in Clinical Medicine) - 330;
· Astashahada ya Maabara za Afya (Technician Certificate in Medical Laboratory Sciences) - 120; na
· Astashahada Sayansi ya Ufamasia (Technician Certificate in Pharmaceutical Sciences) - 20.
Nafasi
hizi zinaombwa kupitia mfumo wa pamoja wa kupokea na kuchakata maombi
(CAS). Muombaji atatakiwa kupitia orodha ya wilaya zenye nafasi za ajira
kwa fani anayotaka kujiunga nayo na iwapo utafanikiwa kupata udhamini
wa masomo kwa fani uliyoomba utatakiwa kujaza fomu ya mkataba wa ahadi
(Bonding) ya kufanya kazi katika eneo ulilochagua baada ya kuwa
umehitimu mafunzo.
7. Utaratibu wa kutoa taarifa kwa waliochaguliwa:
a)
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa pamoja na NACTE watakuwa na
wajibu wa kuwataarifu wale wote watakaofanikiwa kuchaguliwa kujiunga na
kozi mbalimbali kupitia anuani zao za barua pepe, magazeti, ‘website’ ya
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na NACTE.
b) Taarifa hizo zitatumwa pia kwenye kanda za mafunzo na vyuo vyote vya mafunzo haya.
8. Muda wa mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 30 June, 2014.
9. Muhula wa masomo unatarajiwa kuanza tarehe 27 Oktoba, 2014.
Imetolewa na:
KatibuMkuu,
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
S.L.P.9083,
Dar es Salaam.
Hii miaka katika hizi sentensi ni sahihi?
ReplyDeleteii. Awe amemaliza kidato cha nne kati ya mwaka 2009 na 2013, sifa hii inatumika kwawanaotaka kujiunga katika vyuo vya serikakli tu
iii. Cheti chake cha kidato cha nne, kionyeshe ufaulu wa jumla usiopungua point 28 kwamatokeo ya mwaka 2012 kurudi nyuma na point 35 kwa matokeo ya mwaka 2013.
8. Muda wa mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 30 June, 2014.
9. Muhula wa masomo unatarajiwa kuanza tarehe 27 Oktoba, 2014.
hivi utaratibu upoje kwa wanaotaka kujiunga mwaka huu wa 2015
ReplyDeleteNaomba kuelekezwa jinsi ya kupata hizo form ?
Deletehivi utaratibu upoje kwa wanaotaka kujiunga mwaka huu wa 2015/2016
ReplyDeleteJe nafasi zipo kwa mwaka 2016
ReplyDeleteivi nikiwa na D ya chemia na D ya bioz na weza kupata chuo cha afya kweli
ReplyDeletejaman nna c ya chemia c ya bios na c ya geo c ya english na d ya maths naweza kujiungaa na muhimbili university of health
ReplyDeletejaman nna c ya chemia c ya bios na c ya geo c ya english na d ya maths naweza kujiungaa na muhimbili university of health
ReplyDeleteni matokeo ya CSEE ama ACSEE?
Delete