Habari Zetu :

Home » » BALALI BADO YUKO HAI

BALALI BADO YUKO HAI

Written By Unknown on Thursday, November 29, 2012 | 2:48 PM

    BALALI AIBUKIA TWITTER AKIMHUSISHA ZITTO NA ANGUKO LA CHADEMA


Wote tunafahamu kuwa aliyekuwa gavana wa benki kuu ya Tanzania Daudi Balali alifariki dunia tarehe 16.05.2008 huko Boston, Marekani na kuzikwa huko huko.


Lakini kwa watumiaji wa Twitter watakuwa wanamfahamu Daudi Balali wa kwenye mtandao huo ambaye ameendelea kumuumiza vichwa vya watu wengi kuwa ni nani huyu aliye nyuma ya akaunti hiyo na akiendelea kudai kuwa bado yupo hai? 


October 1 alitweet, “Nitakutana na Rais Kikwete na ujumbe wake wiki hii hapa Marekani."

Anavyoonekana ni msomi haswaa na anaishi nje ya nchi. Ni mtu makini, ana hoja, anaijua siasa ya Tanzania na yupo consistent! Hivi karibuni mtu huyo alidai kuwa amekuja Tanzania na kulala kwenye hoteli iliyo karibu na ofisi yake ya zamani.


“In Dar es Salaam, Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kempinski Kilimanjaro Hotel. Feels good to be close to my former office, BoT,” alitweet November 13.

Kutokana na kile anachokiandika anaonekana kuwa ni kada mzuri wa CCM na leo ameibuka na kutabiri anguko la CHADEMA kwa kutweet, “Chadema will die by disintegration. Zitto Kabwe and 3 other prominent members will move to CCM,the rest will form 2 new political parties."

Anasema CHADEMA itavunjika ambapo Zitto Kabwe na wanachama wengine watatu wa chama hicho watahamia CCM na wengi wataanzisha vyama viwili vipya vya siasa.
Hata hivyo anadai ameamua kuondoka nchini mapema na kurudi Gaithersburg, Maryland kutokana kuhofia usalama wake.

“I am leaving Dar es Salaam tonight instead of Wednesday on security reasons.”

Mwisho ameendelea kusisitiza kuwa kweli yupo hai kwa kutweet:

I AM REAL. TAKE IT OR LEAVE IT. TWITTER IS THE MESSENGER. THE SURPRISE IS YET TO COME.

Ni nani huyu??????.......
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

PROFESSIONAL BLOG DESIGNERS

PROFESSIONAL BLOG DESIGNERS

IDADI YA WATU

BLOG ARCHIVE

DROP YOUR COMMENTS HERE

 
Designed by : Bongo Blogs Designers | Bloggerized by | Tryphone Chasama Jr
Contacts: 0719 625003 / 0765 860437Welcome
Copyright © 2011. SNOUT HOT NEWZ - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template