Habari Zetu :

Home » , » SCOLARI KUBAKIZA KOMBE LA DUNIA BRAZIL

SCOLARI KUBAKIZA KOMBE LA DUNIA BRAZIL

Written By Unknown on Thursday, November 29, 2012 | 2:16 PM

                         Felipe Scolari akabidhiwa Brazil
                                               Louis Felipe Scolari
Felipe Scolari amechaguliwa kuiongoza Brazil katika kombe la Dunia huko Brazil. Scolari aliiongoza Brazil katika ushindi wao wa mwaka 2002 na sasa ataiongoza timu hiyo ya taifa ambayo ina vikombe vitano vya Dunia katika michuano itayofanyika mwaka 2014 .
Bosi huyo wa zamani wa Chelsea alikuwa hana kazi tangu alipoondoka Palmeiras in Septemba, pia aliiongoza Ureno 2006 katika kombe la dunia na mwaka 2004 na 2008 katika Kombe la mataifa ya Ulaya.
Scolari amefurahia kuchaguliwa kwake katika kuiongoza timu hiyo.
Uteuzi huo umeenda sambamba na kuteuliwa kwa Pereila kuwa mkurugenzi wa ufundi katika timu ya taifa ya Brazil ili kuweka nguvu katika kuandaa timu ambayo italibakiza kombe la dunia katika ardhi ya nyumbani.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

PROFESSIONAL BLOG DESIGNERS

PROFESSIONAL BLOG DESIGNERS

IDADI YA WATU

BLOG ARCHIVE

DROP YOUR COMMENTS HERE

 
Designed by : Bongo Blogs Designers | Bloggerized by | Tryphone Chasama Jr
Contacts: 0719 625003 / 0765 860437Welcome
Copyright © 2011. SNOUT HOT NEWZ - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template