Abdallah Bulembo Majura
KUNDI
linalodaiwa kuwa la wafuasi wa Chama cha Demockrasia na Maendeleo Chadema juzi lilivamia Mkutano wa
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Abdallah Bulembo na kufanya
vurugu ambazo zilisababisha watu kadhaa kujeruhiwa.
Vurugu hizo zilitokea kwenye mkutano ulioandaliwa kwa ajili ya mwenyekiti huyo katika Mji wa Mlandizi, Mkoa wa Pwani.
Mwenyekiti huyo ambaye hivi sasa yuko ziarani
mkoani Pwani juzi alipangiwa azungumze na wakazi wa mji huo juu ya
masuala mbalimbali, lakini muda mfupi alipowasili uwanjani hapo mambo
yalibadilika ghafla na kuanza kwa vurugu hali iliyosababisha kutoweka
kwa amani katika eneo hilo .
Akiwa na baadhi ya viongozi wa ngazi
mbalimbali, Bulembo aliwasili katika viwanja hivyo saa 11:00 baada ya
kuketi ndipo mawe yalianza kurushwa kutoka nje ya uwanja kuelekea maeneo
walikokuwa wameketi wanachama wa CCM pamoja na watu wengine
Hali hiyo ilidumu kwa takribani saa moja huku
baadhi ya wanachama wa pande mbili wakionekana wakiwa katika mvutano na
kurushiana makonde na kugombea bendera ambapo wa upande wa Chadema
walikuwa wakipora bendera za CCM jambo lililowafanya nao wa CCM waanze
kupora bendera za Chadema.
Katika kipindi chote hicho mwenyekiti huyo
alionekana akiwa ameketi pamoja na baadhi ya viongozi wa ngazi ya wilaya
na mkoa huku wanachama wa pande mbili wakiendelea na mvutano mkali
ambapo watu watatu walijeruhiwa na kupelekwa katika Kituo cha Afya
Mlandizi na baadaye kupelekwa Hospitali ya Tumbi kwa ajili ya matibabu.
Baada ya hali ya vurugu kupungua katika eneo
hilo ndipo viongozi mbalimbali wa (CCM) walianza kupanda jukwaani tayari
kwa kuanza kuzungumza huku wakiwatupia lawana polisi kwa kile
walichoeleza kuwa hawakuwajibika ipasavyo katika kutuliza vurugu hizo.
“Napenda kusema kuwa watuwaliotufanyia fujo
wapo mpaka sasa hapa uwanjani na tumesha watambua kwa majina na mahali
wanapoishi na tutahakikisha wanakamatwa na sheria inachukua mkondo
wake,” alisema.
Aidha ilidaiwa kuwa katika vurugu hizo
jenereta lililokuwa likitumika kwenye mkutano huo kama chanzo cah umeme
lilipotea katika mazingira ya kutatanisha pamoja na bendera za wanachama
wa CCM.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !