MAUAJI KANO, NIGERIA
Written By Unknown on Friday, February 8, 2013 | 10:36 PM
Ripoti kutoka nchini Nigeria zinasema kuwa watu 12 wakiwemo wafanyakazi waliokuwa wanatoa chanjo ya Polio kwa watoto, wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.
Maafisa wa afya wameiambia BBC kuwa wafanyakazi wanane waliokuwa wanatoa chanjo waliuawa mjini Kano,na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Walioshuhudia mauaji hayo wanasema kuwa, watu wengine 8 waliuawa katika kituo cha afya maeneo ya Hotoro, karibu na mji wa Kano.
Miongoni mwa waliouawa ni wanawake waliokuwa wanawasubiri watoto wao, waliokuwa wanachanjwa.
Baadhi ya viongozi wa kiisilamu, Kaskazini mwa Nigeria wamekuwa wakipinga chanjo ya Polio, wakisema inasababisha watu kukosa uwezo wa kuzaa.
Source; BBC
Labels:
mchanganyiko,
mpya
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !