Oscar Pistorius katikati akiwa na maofisa usalama.
Oscar Pistorius akiwa na aliyekuwa mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini na nyota wa
Olimpiki,Oscar Pistorius, amefikishwa mahakamani akikabiliwa na madai
ya kumuua mchumba wake baada ya kupigwa risasi akiwa nyumbani kwa
Pistorius mjini Pretoria.
Baada ya kufikishwa mahakamani, wakala wa Oscar alikanusha madai hayo vikali.
Ombi la dhamana ya mkimbiaji huyo limeahirishwa hadi Jumanne wiki ijayo,na kwamba yuko mbaroni sasa.
Mwaka jana Pistorius alikuwa mwanariadha wa kwanza mlemavu kuruhusiwa kushindana na wanariadha wengine wasio na ulemavu kwenye michezo ya Olimpiki, kwa kutumia miguu bandia.
Pistorius alikuwa mkimbiaji wa kwanza mlemavu kuruhusiwa na shirika la kimataifa la riadha kuweza kushindana na wanaridha wengine wasio na ulemavu wowote. Duru zinasema kukamatwa kwa Pistorous kumewashangaza wengi sana Afrika Kusini ambako anatazamiwa kama shujaa.
Amekuwa na uhusiano na mchumba wake marehemu, Reeva Steenkamp tangu Novemba mwaka jana, na walijulikana sana kwa kuwa wapenzi wenye kusifika sana nchini humo.Wataalamu wa uchunguzi, wanatarajiwa kuendelea na uchunguzi wao katika nyumba ya Pistorius ambako mchumba wake Steenkamp, aliuawa.
Awali duru zilisema kuwa Pistorius huenda alimuua Reeva Steenkamp kimakosa kwa kudhania kuwa ni mwizi aliyekuwa amemvamia, ingawa polisi walipuuza madai hayo.
Polisi walisema kuwa kumekuwa na visa kadhaa vilivyoriptiwa kutokea nyumbani kwa Pistorius na kutajwa kuwa ugomvi wa kinyumbani.
Pistorius anasifika kama mwanaridha wa kwanza mlemavu kushiriki michezo ya Olimpiki. Habari za mauaji ya mpenzi wake Pistorius zimewashangaza wengi Afrika Kusini kwani anasifika kama mwanaridha anayeiletea nchi hiyo sifa.
Afrika Kusini ni moja ya nchi zenye visa vingi vya uhalifu duniani na watu wengi wanamiliki silaha za kujilinda
Source: BBC
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !