Uhuru Kenyatta na William Ruto
NAIROBI, KENYA.
Mahakama kuu nchini Kenya imeeleza kwamba haiwezi
kuamua iwapo Uhuru Kenyatta na William Ruto wanapaswa kugombea nyadhifa
katika uchaguzi mkuu ujao ama la. Wawili hao wanakabiliwa na tuhuma za kuchochea
ghasia nchini Kenya baada ya uchaguzi uliokumbwa na utata na kusababisha
mapigano ya kikabila.
Ikiwa zimesalia wiki mbili tu kwa
uchaguzi mkuu kufanyika Kenya, inaonekana kuwa wananchi ndiyo
watakaoamua kupitia kura, iwapo Uhuru Kenyatta na William Ruto wanafaa
au hawafai kuwa viongozi nchini. Uhuru Kenyatta anawania urais katika uchaguzi mkuu utakaokuja katika muda wa wiki mbili zijazo na makamu wake ni William Ruto.
Kesi hiyo iliwasilishwa na mashirika yasiyo ya
serikali yaliyotaka kubainishiwa iwapo viongozi hao wawili wa muungano
wa kisiasa, Jubilee, wana uwezo wa kuhudumu katika ofisi ya serikali
wakati wanatuhumiwa kwa kesi za uhalifu. Hali hiyo yanaiona mashirika hayo kuwa ni kwenda kinyume na katiba ya nchi.
Mahakama ilikuwa iangalie iwapo Uhuru na Ruto
wangechaguliwa, wataweza kutimiza jukumu la kuiongoza nchi, wakati
wanatuhumiwa kwa kuhusika na ghasia zilizoshuhudiwa Kenya baada ya
uchaguzi mkuu wa mwaka 2007, katika mahakama ya uhalifu ICC, mjini Hague
Uholanzi.
Mahakama inajaribu kuona iwapo Uhuru na Ruto
ikiwa watachaguliwa wataweza kutimiza jukumu la kuiongoza nchi, na
wakati huo huo kukabiliana na kesi inayowaandama katika mahakama ya
uhalifu wa kivita ICC mjini Hague Uholanzi, ambapo wanatuhumiwa kuhusika
na ghasia zilizoshuhudiwa baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.
Uamuzi huu umetolewa baada ya hapo jana kuwepo
kikao cha mahakama hiyo ya uhalifu ICC, kukagua hali ya kesi hiyo
inayowakabili wawili hao.Kesi hiyo iliyowasilishwa na mashirika yasiyo ya
kiserikali inaendelea katika mahakama kuu mjini Nairobi na inatarajiwa
kutoa uamuzi iwapo mahakama ina uwezo wa kutoa uamuzi juu ya wawili hao
au iwapo itahitaji usaidizi wa mahakama ya juu nchini kufikia uamuzi
kuhusu hilo. Zimesalia wiki mbili tu kwa uchaguzi mkuu kufanyika Kenya na uamuzi huu huenda ukawa na athari kubwa kwa uchaguzi ujao.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !