Habari Zetu :

Home » » SHARO MILIONEA AFARIKI DUNIA

SHARO MILIONEA AFARIKI DUNIA

Written By Unknown on Tuesday, November 27, 2012 | 12:33 PM


 
 
KOMEDIAN ambaye pia alikuwa msanii wa muziki wa Bongofleva, Hussein Mkieti ‘Sharo Milionea’ amefariki dunia leo majira ya saa mbili usiku katika ajali ya gari. Sharo amefikwa na mauti wakati akiwa safarini akitokea Dar es Salaam kuelekea nyumbani kwao, Kijiji cha Lusanga, Muheza mkoani Tanga. Msanii huyo alikuwa anaendesha gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T478 BVR na amepata ajali eneo la Songa- Maguzoni wilaya ya Muheza mkoani Tanga. Marehemu alikuwa peke yake kwenye gari. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Costantine Massawe amethibitisha kutokea ajali hiyo na katika taarifa yake kwa vyombo vya habari saa chache baada ya ajali,  alisema kuwa mchoro wa ajali unaonesha kuwa gari la marehemu liliacha njia kabla ya kupinduka mara kadhaa. Naye Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Subira Mgalu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kubainisha kwamba gari alilopata nalo ajali limeharibika sana.

“Mimi sijafika eneo la tukio lakini nimezungumza na OCD wetu hapa Muheza, Andrew Satta yeye alifika eneo la tukio na kunipa taarifa kamili. Ukweli ni kwamba msiba huu ni majonzi na pigo kubwa kwa Wilaya ya Muheza kwa sababu huyu kijana ni mzawa wa hapa.
“Muheza tulikuwa tunajivunia kipaji cha Sharo Milionea lakini hatuna jinsi, kila kitu kinapangwa na Mwenyezi Mungu,” alisema Mgalu.
 
Tanzania has lost another irreplaceable talent, Gone too soon. R.I.P Sharo Milionea
 Hivi ndivyo linavyo onekana gari aina ya Toyota Harrier alilokuwa anaendesha marehem Ramadhan Hassan aka Sharo Milionea mara baada ya kupata nalo ajali na kusababisha kifo chake.
Hivi ndivyo gari hilo inassemekana linavyo onekana kwa mbele 
(naomba mtuwie radhi imebidii tuondoe ile picha ya text maana inaelekea kuna mtu kaamua kujifurahishia na ujitunguia sms ionekane alikuwa anachat na marehemu lakini alikosea mda maana mda ulioweka tayari ndugu yetu alikuwa amesha angulia mbele za haki)
 
                        Mwili wa marehemu Sharo mara baada ya ajali

HIKI NDO ALICHOKISEMA KAMANDA WA POLISI MKOA WA TANGA KUHUSU KIFO CHA SHARO MILLIONEA

Taarifa Kuhusu kifo cha msanii/mwigizaji Sharo Milionea, namkariri Kamanda wa Polisi Tanga akisema “leo majira ya saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera Muheza mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo la Maguzonizonga wilayani Muheza hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza” Kamanda amesema hakuna kona kali sana wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali Sharo Milionea, katikati ya Segera na Muheza ambapo gari imehifadhiwa mahali salama kwa sababu haitembei.Kwenye gari alikua mwenyewe

YANAYOJIRI KWENYE MSIBA WA SHARO MILLIONEA: 

Hali ya mzee King Majuto presha imepanda na hali kuzidi kuwa mbaya kutokana na kupata taarifa za msiba wa Sharo Milionea.



Mjomba wa marehemu Sharo Millionea, Bwana Omary Fundikira asema marehemu anatarajiwa kuzikwa siku ya kesho, Jumatano. Hii ni kutokana na msanii mwenzake John Maganga kuzikwa leo.




Mkuu wa polisi mkoa wa Tanga RPC Costantine Massawe asema Hussein Ramadhani (Sharo Milionea) alikuwa mwenyewe katika gari na ilipotokea ajali gari lilimrusha nje na kufariki hapohapo.




Pia rafiki wa marehemu bwana Mohamed Ismail ambaye ndiye aliyemuazimisha gari alilopata nalo ajali, asema ilitakiwa waongozane kwenda Tanga pamoja ila alishindwa maana alipata majukumu mengine.











Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

PROFESSIONAL BLOG DESIGNERS

PROFESSIONAL BLOG DESIGNERS

IDADI YA WATU

BLOG ARCHIVE

DROP YOUR COMMENTS HERE

 
Designed by : Bongo Blogs Designers | Bloggerized by | Tryphone Chasama Jr
Contacts: 0719 625003 / 0765 860437Welcome
Copyright © 2011. SNOUT HOT NEWZ - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template