Kumekuwa na matatizo kadhaa kwa watumiaji au wale wanaotaka kuweka bidhaa za kaspersky kwenye kompyuta zao.
Huu ni msaada mfupi wa kukabiliana na baadhi ya matatizo.
Huu ni msaada mfupi wa kukabiliana na baadhi ya matatizo.
1 – WINDOWS 8
Kwa wale wanaonunua kaspersky antivirus au internet security kwenye maduka ya nchi za afrika mashariki wameona kwamba programu iliyopo kwenye cd haiwezi kuingia kwenye windows 8, matukeo yake ni kutupa cd hizo na kutafuta antivirus nyingine.
Ni kwamba matoleo mengi ya kaspersky yaliyopo dukani sasa hivi
yalinunuliwa kabla windows 8 kutoka na hayana updates kwa ajili ya windows 8.
Unachotakiwa kufanya kama unaweza tembelea tovuti ya kaspersky au
tovuti yoyote yenye programu mpya ya kaspersky utaweza kudownload bure utaingiza kwenye kompyuta yako na utaweza kutumia keys zile zile uliyonunulia antivirus yako.
2 – MAJIRA SAHIHI
Baadhi ya watu huwa wanaweka majira ambayo sio sahihi kwenye kompyuta zao ili kuepuka kushtukiwa kwenye masuala ya leseni kama za windows, Microsoft office na nyingine nyingi.
Unapokuwa na majira ambayo sio sahihi kaspersky haitoingia au
haitofanya kazi kwa usahihi kwa sababu haitoweza kupata uwezesho
sahihi kutoka kwenye server ili iweze kuwa bora zaidi.
haitofanya kazi kwa usahihi kwa sababu haitoweza kupata uwezesho
sahihi kutoka kwenye server ili iweze kuwa bora zaidi.
3 – MAHITAJI SAHIHI
Kaspersky haswa hii ya 2013 ni kubwa kitogo katika kuingiza na
ufanyaji kazi, kwahiyo inahitaji kompyuta kuwa na viwango sahihi ili kuweza kuingiza bidhaa hii na ili iweze kuwa nyepesi na ya haraka katika kutekeleza majukumu ya kulinda kompyuta yako.
Tafadhali angalia kompyuta yako kama inaviwango vinavyotakiwa na
kaspersky ili iweze kuingiza.
Mfano RAM inatakiwa iwe zaidi ya GB 1
4 – UPDATES ILI KUBORESHA
Wengi wetu huwa tunajisahau kufanya updates za mara kwa mara kwenye kompyuta zetu haswa antivirus, matokeo yake ni kuvamiwa na virus au kushambuliwa na kuharibika kwa programu au kompyuta yenyewe.
Tafadhali unapopata kaspersky 2013 fanya updates kwa asilimia 100 muda huo kama unaweza, kisha uwe unaangalia updates za mara kwa mara ambazo zinaingia moja kwa moja.
5 – KUTUMIA ANTIVIRUS MBILI AU ZAIDI
Unaweza kutumia kama unajua kile unachofanya lakini sikushauri, pia sio
antivirus zote zinakubali kuingia ambapo kuna moja nyingi
zitakuuliza kama unataka kuondoa moja ili hiyo unayoingiza iingie
nyingine hazina tatizo hilo.
Tatizo la antivirus ni kwamba hamna ambayo iko vizuri kwa asilimia 100, nyingine zina matatizo Fulani katika utekelezaji wa baadhi ya majukumu au ni rahisi kushambuliwa na kuacha kufanya kazi.
zitakuuliza kama unataka kuondoa moja ili hiyo unayoingiza iingie
nyingine hazina tatizo hilo.
Tatizo la antivirus ni kwamba hamna ambayo iko vizuri kwa asilimia 100, nyingine zina matatizo Fulani katika utekelezaji wa baadhi ya majukumu au ni rahisi kushambuliwa na kuacha kufanya kazi.
Kwa ushauri zaidi kuhusu kaspersky au antivirus nyingine piga
+255759282766 au samuelsnout@gmail.com
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !