Habari Zetu :

Home » » IVORY COAST WATWANGANA UWANJANI

IVORY COAST WATWANGANA UWANJANI

Written By Unknown on Saturday, June 15, 2013 | 7:58 AM




IVORY COAST wamepagawa. Dakika chache kabla hawajapanda ndege na kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam juzi Alhamisi usiku, mastaa wawili wa timu hiyo, Jean-Jacques Gosso Gosso na kinda wa Manchester City, Abdul Razak walitiana ngumi wakiwa katika uwanja wa mazoezi na mmojawapo alitimuliwa.
Ivory Coast itacheza na Taifa Stars kesho Jumapili katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia saa 9:00 alasiri.
Bila ya kujua chanzo cha ugomvi huo katika Uwanja wa Felix Houphouet Boigny, Gosso Gosso anayekipiga katika klabu ya Mersin Idmanyurdu ya Uturuki alionekana akiwa amemkaba kabali Razak ambaye inasemekana ndiye chanzo cha ugomvi huo.
Kiungo Yaya Toure ambaye alilikosa pambano lililopita dhidi ya Taifa Stars Juni mwaka jana nchini Ivory Coast alionekana kupumbazwa na ugomvi huo uliotokea karibu yake ambao ulimuhusu kinda wao wa Manchester City ambayo imekuwa ikikumbwa na kashfa ya ugomvi wa mazoezini mara kwa mara.
Kutokana na ugomvi huo,Razak ameondolewa katika kambi ya Ivory Coast na hakusafiri na wenzake katika kikosi kilichotua Dar es Salaam  kwa ndege ya kukodi.
Kwa Toure, hilo linaendelea kuwa tukio jingine mbele ya macho yake linalomuhusu mchezaji wa Manchester City.
Katika uwanja wa mazoezi wa klabu yake kwa nyakati tofauti amewahi kuwashuhudia mastaa wa Man City kama vile, Mario Balotelli, Jerome Boateng, Micah Richards na hata kocha wa zamani, Roberto Mancini wakijihusisha na ugomvi.

Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

PROFESSIONAL BLOG DESIGNERS

PROFESSIONAL BLOG DESIGNERS

IDADI YA WATU

BLOG ARCHIVE

DROP YOUR COMMENTS HERE

 
Designed by : Bongo Blogs Designers | Bloggerized by | Tryphone Chasama Jr
Contacts: 0719 625003 / 0765 860437Welcome
Copyright © 2011. SNOUT HOT NEWZ - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template