Home »
mchanganyiko
,
mpya
» MWENYEKITI NA KATIBU WA NECTA KUJIUZURU ENDAPO SERIKALI ITABADILISHA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE
MWENYEKITI NA KATIBU WA NECTA KUJIUZURU ENDAPO SERIKALI ITABADILISHA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE
Written By Unknown on Wednesday, May 8, 2013 | 8:06 PM
Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani la Taifa-NECTA ambaye pia ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Prof.Rwekaza Sympho Mukandala amesema hayuko tayari kubadili matokeo ya Kidato cha Nne.
Chanzo cha karibu cha Prof.Mukandala kinadai kuwa mara baada ya kutolewa taarifa ya Serikali inayotaka 'kuboreshwa' kwa matokeo hayo,Prof.Mukandala ameonesha kukataa amri hiyo hadi sasa. 'Sisi tulipitisha matokeo hayo mbele yao na kwa idhini yao.
Iweje leo Baraza libadili matokeo?.Tunafanya hivi kwa faida ya nani na kwa ustawi wa elimu ya wapi?' alinukuliwa akihoji Prof.Mukandala.
Habari za kuaminka zinadai kuwa Prof.Mukandala pamoja na Katibu Mtendaji Dr.Joyce Ndalichako wanajiandaa kuachia ngazi kama Serikali itasimamia uamuzi wake huo.
Labels:
mchanganyiko,
mpya
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !