Mwanzoni mwa mwezi huu Lady Jaydee aliamua kuibuka na kuituhumu Clouds Media Group kwa kutumia mitandao ya kijamii kama facebook, twitter nab log yake kwamba wana muhujumu kimuziki , kuzuia matangazo ya mgahawa wake wa Nyumbani Lounge na kipaji chake kwa ujumba tuhuma ambazo Ruge na Clouds wanazikanusha vikali.
Wadau mbalimbali wamejitokeza kulizungumzia sakata hilo ikiwa ni pamoja na Naibu Waziri wa Habari Michezo
Vijana na Utamaduni Amos Makala ambaye alitangaza hadharani kulivalia njuga
suala la mzozo kati yapande hizo mbili.
Tanzania
Daima ambayo ilimpigia simu Ruge na kumuuliza ana lipi la kusema baada
ya Makala kutamka kwamba atawaita wawili hao na kuzungumza nao sambamba
na kuleta suluhu.
“Mimi kana nilivyosema katika tamko langu wiki iliyopita kwamba niko tayari tuitwe na watu watusikilize pande zote mbili hasa
mlalamikaji na ukweli uweze kuwa wazi zaidi kwa sababu hadi sasa Lady
Jaydee amekuwa akisema mambo mengi kiasi kwamba hata nashindwa
kumuelewa”
Na siyo Waziri Makalla tu pia ikiwezekana hata kama
kuna watu wengine wanataka kujitokeza ili kutuweka katika kiti moto
watuulize maswali na kila mmoja wetu aote majibu mbele ya hao watu mimi
niko radhi kufanya hivyo” anasema Ruge.
Wakati huohuo Ruge ameongeza kwamba tayari
ameshafuata taratibu za kisheria ikiwa ni pamoja na kumfungulia
jalada la malalamiko ya kutukanwa na Lady Jaydee na taarifa hiyo
amepelekewa msanii huyo akiitwa katika vyombo vya sheria.
Habari hizo zilithibitishwa na Jide kupitia twitter na facebook aliandika post hii
“Ratiba ya Usiku wa leo ni MACHOZI BAND kama kawaida, ila ratiba ya
Jumatatu natakiwa Mahakama ya Kinondoni..Taarifa zaidi zitafuata nikijua
kinachoendelea....
Ila kwa leo mje tuburudike Nyumbani Lounge mpk asubuhi.”
Ila kwa leo mje tuburudike Nyumbani Lounge mpk asubuhi.”
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !