Nairobi Kenya.
Uhuru Kenyatta wa muungano wa JUBILEE ametangazwa rasmi na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya IEBC Isaac Hassan kuwa mshindi wa urais katika uchaguzi mkuu uliofanyika jumatatu ya tarehe 4/3/2013. Matokeo hayo yametangazwa baada ya majadiliano ya muda mrefu yaliyofanyika kati ya tume ya uchaguzi na mipaka na viongozi wa vyama vilivyokuwa vikiwania nafasi hiyo. Matokeo hayo yamemwacha haamini mpinzani wake mkuu Raila Odinga wa muungano wa CORD.
Jumla ya kula zilizopigwa ni 12,338,667 kati ya wapiga kura 14,337,399 waliojiandikisha na waliokuwa na haki ya kupiga kura. Kenyatta amepata jumla ya kura 6,173,433 ambazo ni sawa na asilimia 50.03 dhidi ya mpinzani wake Odinga aliyepata kura 5,340,399 sawa na asilimia 43 ya kula zote. Matokeo hayo ndiyo yaliyomfanya Uhuru kutangazwa rasmi kuwa rais mteule wa awamu ya nne katika Jamhuri ya Watu wa Kenya,
Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta
MATOKEO KWA UJUMLA NI KAMA IFUATAVYO;
1. Uhuru Kenyatta, JUBILEE 6,173,433
2. Raila Odinga, CORD 5,340,399
3. Musalia Mudavadi, AMANI 483,981
4. Peter Kenneth, EAGLE 72,786
5. Abduba Dida, ARK 52,848
6. Martha Karua, NARK-K 43,881
7. James Kiyiapi, RBK 40,998
8. Paul Muite, SAFINA 12,580
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !