Wagombea uraisi nchini Kenya
Wagombea
urais nchini Kenya kwa mara ya kwanza walikutana Jumapili wakati
wa maombi ya kitaifa jijini Nairobi na kuhimiza amani nchini wakati wa
uchaguzi Mkuu utaofanyika siku ya Jumatatu juma lijalo.
Wakati hayo yakijiri wakenya walishiriki katika upigaji kura wa
majaribio kote nchini zoezi ambalo tume huru ya uchaguzi ilisema
ilikuwa fursa ya kuwaonesha wakenya namna watakavyopiga kura.
Zoezi hilo lililoandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi IEBC, linalenga kupunguza dosari za kuharibika kwa kura wakati wa uchaguzi ambapo Raia waishio katika kata zaidi ya 1000 nchini humo
zoezi hilo limepokelewa vizuri na Raia nchini humo wakikiri kupata manufaa ya kufahamu namna ya kufuata taratibu za kupiga kura kwenye uchaguzi ujao, huku wengine wakisema kuwa taratibu za kufuata zimekuwa zikiwakanganya.
Zimesalia siku tatu Raia wa nchi hiyo kutumia haki yao ya msingi ya kikatiba kupiga kura ambapo uchaguzi huo utafanyika juma lijalo.

0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !