Habari Zetu :

Home » , » VURUGU DAR, MAANDAMANO KUSHINIKIZA DHAMANA YA SHEKH ISSA PONDA

VURUGU DAR, MAANDAMANO KUSHINIKIZA DHAMANA YA SHEKH ISSA PONDA

Written By Unknown on Friday, February 15, 2013 | 9:04 PM

 Baadhi ya waumini wa Dini ya Kiislamu wakirushwa kichura leo Katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dar es Salaam walipokamatwa kwa tuhuma za kuandamana kushinikiza Sheikh Ponda aachiwe kwa dhamana.

SHUGHULI katika Jiji la Dar es Salaam jana zilisimama kwa muda baada ya wafuasi wa Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Issa Ponda, kuandamana huku wakipambana na askari polisi waliotanda katika maeneo mengi ya mji. Wafuasi hao waliotawanywa mara kwa mara na kwa mabomu ya machozi na askari polisi, walitumia stali mpya kuandamana hadi kwenye Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), kufikisha ujumbe wao.
Vurugu hizo za polisi kupambana na waandamanaji hao zilianza mchana baada ya swala ya Ijumaa hadi saa 9:00 alasiri huku mitaa mingi katika jiji la Dar es Salaam ikiwa wazi kutokana na watu wengi kuondoka maeneo hayo. Watu hao waliandamana kushinikiza Ponda ambaye yupo ndani akikabiliwa na kesi ya wizi na uvunjifu wa amani aachiwe kwa dhamana.Wafuasi hao walitokea katika misikiti mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam baada ya swala ya Ijumaa ikiwemo, Kwamtoro, Magomeni na Buguruni kuelekea ofisi za DPP zilizopo barabara ya Ohio na Sokoine eneo la posta wakiwa katika vikundi vidogovidogo, tofuati na mandamano ambayo yamezoeleka kufanyika.
Hata hivyo, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya  Dar es Salaam inawashikilia zaidi ya watu 90 ambao walishiriki kuhamasisha na kufanya maandamano.
Kaimu wa Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Mohamed Msangi alisema kati ya watu hao watawahoji ili kuwabaini wahusika wakuu na kufikishwa mahakamani.
“Kama inavyofahamika wazi kwenye  msafara wa mamba kenge hawakosekani sasa tutawahoji ili tuweze kuwapata wahusika wakuu na tuweze kuwachukulia hatua za kisheria kwani hao ni wavunjifu wa amani,”alisema.
Msangi alisema jeshi hilo lilipiga marufuku maandamano hayo lakini watu hao wamekaidi amri hiyo na kwamba sasa watachukuliwa hatua za kisheria. Alisema kulikuwa na vikundi vya watu katika maeneo ya Buguruni, Mnazi Mmoja na Kariakoo ambao walikuwa katika makundi huku wengine wakiandamana katika makundi.
“Tumeweza kuchukua hatua kwa watu waliyokuwa wanataka kujaribu kuvunja amani kwa kufanya maandamano  kwani tumedhibiti hali hiyo na kuweza kuwakamata watu 80 ambao wapo katika kituo cha Polisi Kati  na Msimbazi,”alisema Msangi.
Alisema hali sasa ni shwali na kwamba vurugu ambazo zilitaka kujitokeza zimedhibitiowa.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

PROFESSIONAL BLOG DESIGNERS

PROFESSIONAL BLOG DESIGNERS

IDADI YA WATU

BLOG ARCHIVE

DROP YOUR COMMENTS HERE

 
Designed by : Bongo Blogs Designers | Bloggerized by | Tryphone Chasama Jr
Contacts: 0719 625003 / 0765 860437Welcome
Copyright © 2011. SNOUT HOT NEWZ - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template