Habari Zetu :

Home » , » ZANZIBAR YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA CHALLENGE

ZANZIBAR YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA CHALLENGE

Written By Unknown on Thursday, November 29, 2012 | 2:00 PM

                            Zanzibar yatinga Robo fainali

Ikiwa imeanza na wachezaji nanewanaocheza ligi kuu ya Tanzania Bara, timu ya Taifa ya Zanzibar ( Zanzibar Heroes) imeungana na timu za Uganda na Burundi, kufuzu kwa hatua ya robo fainali ya michuano ya 38 ya Tusker Challenge Cup.
Zanzibar iliweza kuonyesha soka la nguvu tofauti na walivyocheza mchezo wa ufunguzi dhidi ya Eritrea, jumatatu iliyopita. Ilitumia dakika nane tu kuandika bao lake la kuongoza.
Hamis Mcha Hamis, mtoto wa mwanasoka wa zamani wa Zanzibar na timu ya taifa ya Tanzania, alitumia makosa ya ‘ lazima’ za mlinda mlando wa Rwanda, Jean Claude Ndoli, ambaye aliukosa mpira uliokuwa umepigwa na kiungo-mshambuliaji wa pembeni, Suleiman Kassim Selembe, kutokana na kufanya kosa hilo, Mcha, alifunga bao la kwanza kwa nchi yake katika michuano hiyo. Zanzibar, ambao hawakuonekana kuathiriwa sana na hali ya uwanja wa Namboole, kujaa maji, ingeweza kupata mabao zaidi kupitia kwa mshambuliaji, Seif Abdalah, ambaye alipoteza nafasi kadhaa.

Khamis-Mcha-Khamis

Rwanda2-1Zanzibar(Michuanoiliyopita)
Mwadini Ally Mwadini, aliwapanga vyema walinzi wake, Nassorro Masoud, Nadir Haroub, Aggrey Morris, na Nuhu Samih, na kuibuka nyota wa mchezo, mara kadhaa alitumia mwili wake kuinusuru timu yake isipoteze mchezo, aliuwahi mpira uliokuwa umepigwa na kiungo wa Rwanda, Haruna Niyonzima, ukiwa unaelekea nyavuni, alifanya kazi kubwa katika nafasi yake na hilo lilipelekea jitihada za timu nzima kuzaa matunda. Zanzibar, walikwenda nusu ya kwanza ya mchezo wakiwa mbele kwa bao 1-0.
Waliingia kipindi cha pili wakiwa na tahadhali zaidi, nidhamu yao kama mchezaji mmoja mmoja ilikuwa juu, na kwa pamoja walielekezana kila penye mapungufu. Mchezo wao wa kupasiana haukuonekana sana sababu ya uwanja kutokuwa katika hali nzuri. Walijilinda vizuri, japo walinzi mara kadhaa walipitika, lakini uwezo mzuri wa Mwadini uliwahakikishia ushindi, zikiwa zimebaki dakika 20,Rashid Abdalah, aliifungia, Zanzibar, bao la pili. Baadae, Rwanda wakapata bao lao pekee.
Kwa matokeo hayo, Zanzibar, imekuwa timu ya kwanza kufuzu kwa robo fainali kutoka katika kundi C, na timu ya tatu kufuzu kwa hatua hiyo hadi sasa. Zanzibar, imefikisha pointi nne na kuziacha, Rwanda na Malawi, na pointi zao tatu, tatu, uku Eritrea ikiwa na pointi moja. Mechi za mwisho za kundi hili C, zitachezwa siku ya jumapili kwa Malawi kucheza na Zanzibar, uku, Rwanda ikiwakabili, Eritrea.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

PROFESSIONAL BLOG DESIGNERS

PROFESSIONAL BLOG DESIGNERS

IDADI YA WATU

BLOG ARCHIVE

DROP YOUR COMMENTS HERE

 
Designed by : Bongo Blogs Designers | Bloggerized by | Tryphone Chasama Jr
Contacts: 0719 625003 / 0765 860437Welcome
Copyright © 2011. SNOUT HOT NEWZ - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template