BRAZIL 3-0 SPAIN
Ulikuwa usiku mzuri kwa timu ya taifa ya Brazil kutwaa taji la kombe la mabara dhidi ya Hispania katika uwanja wa Maracana. Nyota hiyo ilianza kuonekana katika dakika ya pili baada ya Fred kuipatia Brazil goli la kwanza. Dakika ya 44 Neymar aliipatia timu yake goli la pili katika dakika ya 44 na dakika tatu baada ya kipindi cha pili kuanza Fred alihitimisha kwa kufunga bao la tatu.
Kabla ya mchezo huo kuanza, watu wengi walikuwa wakiipigia chapuo timu ya Hispania kutwaa ubingwa huo lakini mchezo wa kandanda ni dakika 90 uwanjani. Mabingwa hao wa ulaya mara mbili mfululizo 2008 na 2012 na mabingwa wa dunia 2010, walishindwa kabisa kufurukuta mbele ya Brazil. Katika mwendelezo wa mambo kuwa mabaya kwao, dakika ya 55 Sergio Ramos alikosa mkwaju wa penati. Dakika ya 68 Gerrad Pique alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuonyesha mchezo mbaya kwa Neymar.
Hadi kipenga cha mwisho kinapulizwa, Brazil walikuwa mbele kwa mabao matatu na Hispania sifuri.
Italia wamemaliza mashindano hayo kwa kutwaa nafasi ya tatu baada ya kuilaza timu ya Uruguayi kwa penati 3 kwa 2. Timu hizo zilimaliza dakika 90 kwa kufungana magoli 2-2 na kwenda kwenye muda wa ziada ambapo walishindwa kufungana hivyo kulazimika kupigiana penati.

0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !