Habari Zetu :

Home » , » BRAZIL MABINGWA KOMBE LA MABARA (CONFEDERATIONS CUP 2013)

BRAZIL MABINGWA KOMBE LA MABARA (CONFEDERATIONS CUP 2013)

Written By Unknown on Sunday, June 30, 2013 | 8:57 PM

Screenshot2013-06-30at5

BRAZIL 3-0 SPAIN
Ulikuwa usiku mzuri kwa timu ya taifa ya Brazil kutwaa taji la kombe la mabara dhidi ya Hispania katika uwanja wa Maracana. Nyota hiyo ilianza kuonekana katika dakika ya pili baada ya Fred kuipatia Brazil goli la kwanza. Dakika ya 44 Neymar aliipatia timu yake goli la pili katika dakika ya 44 na dakika tatu baada ya kipindi cha pili kuanza Fred alihitimisha kwa kufunga bao la tatu.

Kabla ya mchezo huo kuanza, watu wengi walikuwa wakiipigia chapuo timu ya Hispania kutwaa ubingwa huo lakini mchezo wa kandanda ni dakika 90 uwanjani. Mabingwa hao wa ulaya mara mbili mfululizo 2008 na 2012 na mabingwa wa dunia 2010, walishindwa kabisa kufurukuta mbele ya Brazil. Katika mwendelezo wa mambo kuwa mabaya kwao, dakika ya 55 Sergio Ramos alikosa mkwaju wa penati. Dakika ya 68 Gerrad Pique alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuonyesha mchezo mbaya kwa Neymar.

Hadi  kipenga cha mwisho kinapulizwa, Brazil walikuwa mbele kwa mabao matatu na Hispania sifuri.

Italia wamemaliza mashindano hayo kwa kutwaa nafasi ya tatu baada ya kuilaza timu ya Uruguayi kwa penati 3 kwa 2. Timu hizo zilimaliza dakika 90 kwa kufungana magoli 2-2 na kwenda kwenye muda wa ziada ambapo walishindwa kufungana hivyo kulazimika kupigiana penati.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

PROFESSIONAL BLOG DESIGNERS

PROFESSIONAL BLOG DESIGNERS

IDADI YA WATU

BLOG ARCHIVE

DROP YOUR COMMENTS HERE

 
Designed by : Bongo Blogs Designers | Bloggerized by | Tryphone Chasama Jr
Contacts: 0719 625003 / 0765 860437Welcome
Copyright © 2011. SNOUT HOT NEWZ - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template