Habari Zetu :

Home » , » MATOKEO KIDATO CHA NNE 2012 KUPANGWA UPYA

MATOKEO KIDATO CHA NNE 2012 KUPANGWA UPYA

Written By Unknown on Friday, May 3, 2013 | 4:08 AM

 
National Examination Council of Tanzania (N.E.C.T.A) - Dar es Salaam, Tanzania
 
Serikali imetangaza uamuzi wa kupanga upya matokeo ya kidato cha nne ya 2012. Uamuzi huo umetangazwa mapema leo bungeni na Waziri William Lukuvi, kwa niaba ya Waziri Mkuu. Uamuzi umetokana na kamati ya waziri mkuu iliyokuwa inachunguza kuhusu matokeo hayo kubaini kuwa matokeo hayo yalipangwa kwa utaratibu tofauti na uliokuwa unatumika zamani.

Tetesi za awali zilieleza kwamba matokeo hayo yalipangwa kwa kuzingatia madaraja haya hapa chini, japo Baraza la Mitihani lilikanusha baadaye kwa kusema kuwa taarifa hizo hazikuwa za kweli:

A = 80%-100%-
B = 65%-79%-
C = 50%-64%-
D = 35%-49%-
F = 0%-34%-

Tume ya Waziri Mkuu imebaini kutumika kwa madaraja tofauti na uataratibu wa awali. Hivyo basi, matokeo yaliyotangazwa hayatatumika tena mpaka yaje yaliyopangwa upya. HakiElimu itatoa taarifa rasmi baadaye kuhusu uamuzi huu wa serikali.

Kila la kheri.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

PROFESSIONAL BLOG DESIGNERS

PROFESSIONAL BLOG DESIGNERS

IDADI YA WATU

BLOG ARCHIVE

DROP YOUR COMMENTS HERE

 
Designed by : Bongo Blogs Designers | Bloggerized by | Tryphone Chasama Jr
Contacts: 0719 625003 / 0765 860437Welcome
Copyright © 2011. SNOUT HOT NEWZ - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template