Habari Zetu :

Home » , , » LADY JAY DEE MATATANI, ATAKIWA MAHAKAMANI JUMATATU

LADY JAY DEE MATATANI, ATAKIWA MAHAKAMANI JUMATATU

Written By Unknown on Saturday, May 11, 2013 | 1:53 AM


Photo



 Mwanzoni mwa mwezi huu Lady Jaydee aliamua kuibuka na kuituhumu Clouds Media Group  kwa kutumia mitandao ya kijamii kama facebook, twitter nab log yake kwamba wana muhujumu kimuziki , kuzuia matangazo ya mgahawa wake wa Nyumbani Lounge   na kipaji chake kwa ujumba tuhuma ambazo Ruge na Clouds wanazikanusha vikali. 


  Wadau mbalimbali wamejitokeza kulizungumzia sakata hilo ikiwa ni pamoja na Naibu Waziri wa Habari  Michezo Vijana na Utamaduni Amos Makala ambaye alitangaza hadharani kulivalia njuga suala la mzozo kati yapande hizo mbili.
Tanzania Daima ambayo ilimpigia simu Ruge na kumuuliza ana lipi la kusema baada ya Makala kutamka kwamba atawaita wawili hao na kuzungumza nao sambamba na kuleta suluhu.
“Mimi kana nilivyosema katika tamko langu wiki iliyopita kwamba niko tayari tuitwe na watu watusikilize  pande zote mbili  hasa mlalamikaji na ukweli uweze kuwa wazi zaidi kwa sababu hadi sasa Lady Jaydee amekuwa akisema mambo mengi kiasi kwamba hata nashindwa kumuelewa”
Na siyo Waziri Makalla tu pia ikiwezekana hata kama kuna watu wengine wanataka kujitokeza ili kutuweka katika kiti moto watuulize maswali na kila mmoja wetu aote majibu mbele ya hao watu mimi niko radhi kufanya hivyo” anasema Ruge. 
 Wakati huohuo Ruge ameongeza kwamba  tayari ameshafuata taratibu za kisheria ikiwa ni pamoja na kumfungulia jalada la malalamiko ya kutukanwa na Lady Jaydee na taarifa hiyo amepelekewa  msanii huyo akiitwa katika vyombo vya sheria. 
Habari hizo zilithibitishwa na Jide kupitia twitter na facebook aliandika post hii
     “Ratiba ya Usiku wa leo ni MACHOZI BAND kama kawaida, ila ratiba ya Jumatatu natakiwa Mahakama ya Kinondoni..Taarifa zaidi zitafuata nikijua kinachoendelea....
Ila kwa leo mje tuburudike Nyumbani Lounge mpk asubuhi.” 
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

PROFESSIONAL BLOG DESIGNERS

PROFESSIONAL BLOG DESIGNERS

IDADI YA WATU

BLOG ARCHIVE

DROP YOUR COMMENTS HERE

 
Designed by : Bongo Blogs Designers | Bloggerized by | Tryphone Chasama Jr
Contacts: 0719 625003 / 0765 860437Welcome
Copyright © 2011. SNOUT HOT NEWZ - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template