Pages

Saturday, March 9, 2013

UHURU KENYATTA ATANGAZWA RASMI KUWA RAIS WA NNE WA KENYA



Nairobi Kenya.
Uhuru Kenyatta wa muungano wa JUBILEE ametangazwa rasmi na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya IEBC Isaac Hassan kuwa mshindi wa urais katika uchaguzi mkuu uliofanyika jumatatu ya tarehe 4/3/2013. Matokeo hayo yametangazwa baada ya majadiliano ya muda mrefu yaliyofanyika kati ya tume ya uchaguzi na mipaka na viongozi wa vyama vilivyokuwa vikiwania nafasi hiyo. Matokeo hayo yamemwacha haamini mpinzani wake mkuu Raila Odinga wa muungano wa CORD. 
Jumla ya kula zilizopigwa ni 12,338,667 kati ya wapiga kura 14,337,399 waliojiandikisha na waliokuwa na haki ya kupiga kura. Kenyatta amepata jumla ya kura 6,173,433 ambazo ni sawa na asilimia 50.03 dhidi ya mpinzani wake Odinga aliyepata kura 5,340,399 sawa na asilimia 43 ya kula zote. Matokeo hayo ndiyo yaliyomfanya Uhuru kutangazwa rasmi kuwa rais mteule wa awamu ya nne katika Jamhuri ya Watu wa Kenya,

Uhuru Kenyatta, on November 19
           Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta

MATOKEO KWA UJUMLA NI KAMA IFUATAVYO;
1. Uhuru Kenyatta, JUBILEE  6,173,433
2. Raila Odinga, CORD      5,340,399
3. Musalia Mudavadi,  AMANI  483,981
4. Peter Kenneth, EAGLE  72,786
5. Abduba Dida, ARK  52,848
6. Martha Karua, NARK-K  43,881
7. James Kiyiapi, RBK   40,998
8. Paul Muite, SAFINA  12,580


Friday, March 1, 2013

PICHA ZA MARC ANTHONY NA KIMWANA WA MIAKA 21










Marc Anthony (kushoto) akiwa na Chloe Green (kulia) wakiwa na watoto mapacha wa Marc ambao amezaa na Jennifer Lopez, Max and Emme

 p

p



 CALIFORNIA, UNITED STATES.
Siku ya jumanne Marc Anthony na rafiki yake mpya wa kike Chloe Green wakiwa mtaani wakati wa sikukuu ya kuzaliwa kwa watoto mapacha wa Marc na J. Lo ambao ni Max and Emme.