Habari Zetu :

Home » , » KUELEKEA UCHAGUZI MKUU NCHINI KENYA

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU NCHINI KENYA

Written By Unknown on Thursday, February 28, 2013 | 12:47 AM

Wagombea wa urais nchini Kenya 
 Wagombea  uraisi nchini Kenya

Wagombea urais nchini Kenya kwa mara ya kwanza walikutana Jumapili wakati wa maombi ya kitaifa jijini Nairobi na kuhimiza amani nchini wakati wa uchaguzi Mkuu utaofanyika siku ya Jumatatu juma lijalo.

Wakati hayo yakijiri wakenya walishiriki katika upigaji kura wa majaribio kote nchini zoezi ambalo tume huru ya uchaguzi ilisema ilikuwa fursa ya kuwaonesha wakenya namna watakavyopiga kura.

Zoezi hilo lililoandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi IEBC, linalenga kupunguza dosari za kuharibika kwa kura wakati wa uchaguzi ambapo Raia waishio katika kata zaidi ya 1000 nchini humo

zoezi hilo limepokelewa vizuri na Raia nchini humo wakikiri kupata manufaa ya kufahamu namna ya kufuata taratibu za kupiga kura kwenye uchaguzi ujao, huku wengine wakisema kuwa taratibu za kufuata zimekuwa zikiwakanganya.

Zimesalia siku tatu Raia wa nchi hiyo kutumia haki yao ya msingi ya kikatiba kupiga kura ambapo uchaguzi huo utafanyika juma lijalo.


Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

PROFESSIONAL BLOG DESIGNERS

PROFESSIONAL BLOG DESIGNERS

IDADI YA WATU

BLOG ARCHIVE

DROP YOUR COMMENTS HERE

 
Designed by : Bongo Blogs Designers | Bloggerized by | Tryphone Chasama Jr
Contacts: 0719 625003 / 0765 860437Welcome
Copyright © 2011. SNOUT HOT NEWZ - All Rights Reserved
Template Design by Creating Website Published by Mas Template