Jana wahadhiri Chuo Kikuu cha Dodoma walifanya mkutano mkuu wa mwaka (General Assembly), pamoja na mambo kadhaa wameazima kuanza mgomo kuanzia kesho alhamisi saa 2 asubuhi.

Tukio hili kwanza limechochewa na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Balozi Mwapachu, wiki iliyopita kwenye baraza la chuo alimtukana Mwenyekiti wa jumuiya ya wahadhiri kwa kumuita Mugabe kwa sababu hataki kuitisha uchaguzi. Na akaamuru kikao kijacho asiingie kama uchaguzi hamna. [Tunaamini wana mpango wa kupandikiza mtu wao]

Kati ya mambo yaliyosababisha wahadhiri hao kubaki Chimwaga kwa ajili ya mgomo ni kama ifuatavyo:

1. Chuo kinadai serikali inawaletea hela kidogo sana, ambazo hazitoshelezi, hivyo wanataka kufanya cost cutting: Kuwanyanganya nyumba wahadhiri wote walio chini ya level ya udaktari,: kuanza kutozwa nauli kwenye mabasi, maarufu kama kitumbo au Zonda, kwa siku 2000, wakati nauli ya daladala kwenda na kurudi ni 600 tu.

Wafanyakazi wote kama huna bima ya afya unajigharamia matibabu. Mwalimu atakayeenda kusoma kukatwa mshahara wake. Pia imepiga marufuku walimu kwenda kusoma nje ya UDOM.

Hali ya kuwa chuo chenyewe hakina wahadhiri kabisa. (TA anafundisha shahada ya kwanza, wahadhiri ambao hata sio madaktari wanafundisha shahada ya uzamili, mtu amemaliza Masters anakwenda kufundisha masters).

Kibaya zaidi wahadhiri walikuwa wakilipwa kwa ajili ya kusimamia mitihani (Invigilation) 15,000 kwa kipindi, na kusahihisha (Marking allowance) 500 kwa script moja. Na hii hela inatokana na ada ya mtihani ambayo hulipwa na kila mwanafunzi tsh 20,000, malipo hayo nayo yamesimamishwa, wakati huo huo wanafunzi badala ya kulipa 20,000 wanatakiwa walipe 40,000 kwenye hiyo proposal mpya.

2. Kwenye baraza la chuo, walitangaziwa Prof. Shaban Mlacha ameongezewa miaka minne na Raisi Jakaya Kikwete. Wahadhiri wanahoji mgomo wa mwaka jana,wa walimu na wanafunzi,waziri Mkuu Mizengo Pinda aliahidi atarudi kuja kutoa ufafanuzi hatua zilizofikiwa na serikali, hajarudi, wala ripoti ya tume alizounda haijatolewa, manunguniko ya wafanyakazi, na wanafunzi hayajafanyiwa kazi kabisa.

Hili limesababisha wastani wa wafanyakazi watatu wakiwemo Prof. na madaktari huacha kazi kila mwezi. Kuanzia July 2011, hadi July 2012, jumla ya wafanyakazi 42 wameondoka chuo kwa sababu mbalimbali ikiwemo kuacha kazi (resignation). Mbaya zaidi kumekuwa na ulipizwaji kisasi wa hali ya juu. Wahadhiri wamefukuzwa sana kazi, na baadhi ya kesi zipo mahakamani.

Kibaya zaidi imethibitika kikwete kawaongezea muda viongozi wote wa chuo. Prof. Kikula alistaafu 15 December 2012, ameongezewa nae mkataba, pamoja na lawama zote. Hili wamelichukulia kama Serikali haiwajibiki na imeonyesha dharau kubwa sana, lakini kibaya zaidi hili limechukuliwa kwenye taswira ya Udini, ambao umekuwa ukikitafuna chuo, kufikia hatua ya kuunda kamati ya kushughulikia suala hilo, ambayo pia inasemekana *ilivunjika bila mafanikio kabla hata ya kuanza kazi.

3. Kumekuwa na maswala ya udini sana, na hili lawama zinaelekezwa kwa Mh. Rais namna ya uteuzi wake lakini na baadae ajira. Na hivyo waislamu kujiwekea territory. Mwenyekiti wa baraza, VC, DVC PFA, Bursar, Afisa Mwajiri Mkuu na baadae kundi kubwa sana la wazanzibari waliletwa kwa kupitia Mkurugenzi wa Stadi za elimu ya juu Dr. Ahmed Ame.

Huu ubaguzi umetutafuna hadi kwa wanafunzi, utauona dhahiri wakati wa uchaguzi, na mwaka jana ghasia hizo za kidini zilipelekea vurugu na wanafunzi kujeruhiwa na mpaka sasa kesi zipo mahakamani zinaendelea.

4. Uongozi wa chuo ulipandikiza watu waliojidai usalama wa taifa, na kuanza kupita kwa viongozi kwa ajili ya kuwatisha kuwaua akiwemo aliyekuwa kiongozi mahiri na machachari, Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi, na Makamu wa Jumuiya ya wahadhiri – UDOM.

Kesi hiyo ipo Polisi na ilisharipotiwa Usalama wa Taifa Mkoa, pamoja na ushahidi wote kuwepo, inasemekana Dr. Shukuru Kawambwa alimuombea msamaha afisa huyo feki (Khalifa Kondo), ambaye mmoja wa ndugu yake inasemekana alitajwa kuhusika kwenye shambulio la Ulimboka (Angalia Mwanahalisi la mwisho). Tuhuma hizi pamoja na kufikishiwa viongozi mbalimbali wa Serikali hayajafanyiwa kazi.

5. Tatizo la mishahara kupunjwa na watu kutopanda madaraja kwa wakati limeendelea kuwa tatizo sugu. Ajira bado taratibu haziko wazi, inasemekana ili uajiriwe Finance Department lazima uwe muislamu. Sijui?? Fika UDOM upate takwimu (Bursar- Mohamed Mwandege, Msaidizi wake Rukia, wengine Chang’a, Mwinyi, Athuman Chamosi na wengine watano wote waislamu), masuala haya ndiyo yanaleta mgogoro kwa kuwa hayana ufafanuzi.

6. Kikubwa uongozi wa chuo umekuwa ukikataa kukutana na wahadhiri, walikutana mara moja baada ya Waziri mkuu kuwaamrisha baada ya hapo, walijibu barua kali sana wakionya wasiitwe tena, barua hiyo ilitoka kwa Naibu Makamu Mkuu wa chuo – Taaluma, utafiti na ushauri), sasa hapa wameazimia hawatatoka chimwaga, ukumbi maarufu kwa ajili ya mapambano hadi viongozi hao waje, na Waziri Mkuu aje awaambie mbona hajawasaidia kutatua matatizo yao?

(Ufafanuzi zaidi: Paul Loisulie, Mwenyekiti Jumuiya ya walimu au Lameck mjumbe kamati ya utendaji, jumuiya ya walimu au Richard Alphone huyu anaweza kukupatia hata baadhi ya documents)

(Kwa upande wa uongozi wa chuo, taarifa hizi wanaweza kutolea ufafanuzi Makamu mkuu wa Chuo Prof. Idris Kikula, Mwenyekiti wa baraza la Chuo Balozi Juma Volter Mwapachu. Kuhusu usalama wa raia feki suala hili liko kwa Regional security Officer RSO)