Mkurugenzi wa makosa ya jinai nchini (DCI) Robert Manumba (mwenye miwani), akitoa taarifa hiyo.Kulia kwake ni IGP Said Mwema. |
Jeshi
la polisi Tanzania limekamata watu watano jijini Dar es Salaam kwa
tuhuma za mauaji ya aliyekuwa kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Alberatus
Barlow na bado linaendelea kuwatafuta watuhumiwa wengine.
Akiongea
na waandishi wa habari jijini Mwanza Mkurugenzi wa makosa ya jinai
nchini (DCI) Robert Manumba amewataja watu hao kuwa ni Muganizi Michael Peter
(36) Mkazi wa Isamilo ambae alikiri kumuua kamanda kwa risasi.
Wengine
ni Chacha Waitara Mwita (50), Magige Mwita Marwa, Bugazi Edward Kusota
na Bhoke Mara Mwita(42). Watuhumiwa hawa walikamatwa jijini Daresalaam baada ya kuwekewa
mtego na kwa ushirikiano kati ya jeshi la polisi na wananchi.
Wanaoshikiliwa na jeshi la polisi jijini Mwanza ni pamoja na Mwalimu Doroth Moses lyimo aliyekuwa na RPC wakati mauaji yakitokea,Felix Felician Minde(50),Philimon Felician(46)maarufu kwa jina la Fumo, Bahati Augustino Lazaro(28) na Amos Magoto(30) maarufu kama Bonge.Watuhumiwa hao watano wanafikisha idadi ya watuhumiwa kumi wanaoshikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za mauaji hayo.
Manumba
alisema kikosi kazi cha upelelezi kilichokuwa chini yake kilijigawa
kwenye makundi matatu, yaani kundi la ukamataji, mahojiano na kundi
jingine la intelejensia ambapo walitumia njia ya kisayansi kwa kufuatia
mitandao ya simu. Na kwamba jeshi hilo limefanikiwa kukamata bunduki
iliyotumiwa kutekeleza mauaji hayo na simu aliyoporwa mwanamke aliyekuwa
amesindikizwa na Kamanda Barlow na bado polisi inasaka radio call
aliyokuwa nayo marehemu.
Marehemu
kamanda Barlow aliuawa usiku wa Oktoba 12 kati ya saa saba na saa nane
eneo la, Kitangiri, Kona ya Bwiru mkoani Mwanza baada ya kupigwa risasi
na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi alipokuwa anamsindikiza Mwalimu
Dorothy Moses nyumbani kwake.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !